Machapisho

CHAMA CHAUMA CHAFANYA MAKUTANO MKOANI MARA

TAARIFA YA CHAMA CHA CHAUMA KIKIWANI MKOANI MARA – TAREHE 4 JUNI 2025 Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) kilifanya ziara rasmi mkoani Mara tarehe 4 Juni 2025, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya chama hicho ya kuimarisha uhai wa chama na kuhamasisha wananchi kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025. Ziara hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa chama Taifa, Mhe. Hashim Rungwe Spunda, pamoja na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kikanda. Viongozi hao walifanya mikutano na wanachama, walitembelea matawi ya chama na kuzungumza na wananchi katika maeneo kadhaa ya wilaya za Musoma Mjini, Bunda, Rorya na Tarime. Katika hotuba yake kwa wananchi wa Musoma, Mhe. Rungwe alisisitiza umuhimu wa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kushiriki kwenye uchaguzi mkuu ujao. Alisisitiza kuwa CHAUMA kimejipanga kuleta mabadiliko ya kweli kwa kushughulikia changamoto za ajira kwa vijana, huduma duni za afya, na kupigania rasilimali za taifa zitumike kwa manufaa ya wananchi w...

MARA CHANNEL TV LIVE

Kalibu Sana kwenye channel yetu